Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbuni yazichukua fasta pointi tatu za FGA Talents

Mbuni FC Arusha Mbuni yazichukua fasta pointi tatu za FGA Talents

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kutoka sare mechi mbili mfululizo hatimaye Mbuni FC imezinduka tena na kupata ushindi baada ya kuichapa bao 1-0 FGA Talents.

Mchezo huo wa Ligi ya Championship ulipigwa mapema leo kuanzia saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha ambapo ulianza kwa kasi huku kila timu ikitaka kupata goli la mapema na kuweza kuondoka na ushindi.

Hata hivyo kukosa umakini kwa safu ya ushambuliaji kwa timu zote ilifanya wadau wa soka Arusha wasubirie hadi dakika ya 38 kuona nyavu zikitikisika baada ya Mbuni FC kufunga bao la kuogoza na la ushindi kupitia Advent Pius.

Baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika kocha wa Mbuni FC, Leonard Budeba amewapongeza wachezaji wake kupambana na kuweza kubakisha alama tatu zote nyumbani.

Amesema mchezo ulikuwa mzuri wametengeneza nafasi nyingi lakini nyota wake wakaitumia moja sasa anaenda kufanyia kazi ili mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania yasijirudie.

"Licha ya kupoteza nafasi nyingi lakini vijana wangu wamepambana lazima niwapongeze kwa ilo sasa tunaenda kujipanga ili mchezo ujao pia tushinde", amesema Budeba.

Kocha wa FGA Talents,Athuman Cairo yeye amesema timu yake imepoteza mchezo kutokana na madhaifu ya mwamuzi wa kati ambayo anaamini hakuwa upande wao.

Amesema mchezo huo umekamilika na mshindi kashapatikana tayari kikubwa sasa ataenda kuandaa timu ili kuweza kupambana na TMA Stars katika mchezo ujao kwani ni muhimu kwao kushinda na kusogea juu katika msimamo.

Ushindi huo imeipandisha Mbuni FC hadi nafasi ya nne kwa pointi 18 ikihishusha Pamba FC ya Mwanza zikiwa sawa kwa pointi huku zikitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa baada ya kucheza mechi 10.

Chanzo: Mwanaspoti