Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbuni FC yaichimba mkwara Ruvu Shooting

Mbuni FC.jpeg Mbuni FC yaichimba mkwara Ruvu Shooting

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya Mbuni FC imetamba kufanya kweli dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa mzunguko wa sita wa Ligi ya Championship itakayopigwa Oktoba 15 mwaka huu jijini Arusha.

Timu hiyo katika mechi tano ilizocheza hadi sasa imekusanya alama 10 baada ya kushinda mechi tatu sare moja sawa na mchezo iliyopoteza, ikifunga mabao saba na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara nne huku ikiwa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo.

Mbuni FC inarejea tena nyumbani baada ya kucheza mechi tatu mfululizo ugenini ikishinda mbili jijini Dar dhidi ya Pan African iliyoshinda (0-1), Cosmopolitan (1-2), kabla ya kupokea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa ndugu zao TMA Stars kwenye dabi ya Arachuga ambayo kikanuni Mbuni ilikuwa ugenini.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Daniel Kirai ameweka wazi kuwa kwa sasa wanaendelea na mazoezi kuhakikisha katika mchezo huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid wanashinda na kuendelea kuwa juu kwenye msimamo.

Amesema wanakwenda kukutana na timu nzuri ambayo imetoka Ligi Kuu lakini Ligi ya Championship yule ambaye anafanya maandalizi vizuri ndie anapata matokeo.

“Sisi hatutohofia hilo kwamba wana timu imetoka Ligi Kuu lakini tutakuja kupambana naamini tutapata matokeo kwa sababu kwanza tutakuwa nyumbani,” anasema Kirai

Ametumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki na wadau wa Soka Arusha kuendelea kuiunga mkono timu yao huku akiwaahidi ushindi katika mchezo huo.

Noadha wa timu hiyo upande wake mchezaji wa timu hiyo, Geoffrey Msemwa amesema kwa upande wao wachezaji wamejipanga vyema kupambana na kuweza kubakisha alama tatu nyumbani baada ya kupoteza mchezo uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti