Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge awaombea mishahara wachezaji Ligi Kuu

Mbunge Pic Mbunge wa Makete, Festo Sanga

Tue, 7 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mbunge wa Makete, Festo Sanga amependekeza Serikali kuweka viwango vya mishahara stahiki kwa wachezaji Tanzania kwa madai kuwa wanafanya kazi nzuri lakini malipo yao ni kidogo.

Sanga ametoa kauli hiyo jana Juni 6, 2022 bungeni wakati akichangia kwenye hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mbunge huyo amesema kuna wachezaji wanacheza kwa nguvu wakivuja jasho la damu lakini kinachosikitisha ni kuwa wanalipwa Sh200,000 tu jambo linalomfanya mchezaji akiugua kuwa kwenye wakati mgumu hata kuanza kuchangiwa.

Hata hivyo Sanga amezungumzia zaidi mshahara huo kwa kuutaja mchezo wa mpira wa miguu akiwazungumzia wachezaji wa ligi kuu.

“Mimi napendekeza kwa wachezaji wa ligi kuu kwamba tuweke utaratibu angalau kima cha chini cha mshahara kiwe hata Sh1 milioni ili tuweze kuwaokoa hata kwenye matatizo madogo madogo kwani naamini kuwa inawezekana,” amesema Sanga.

Amemuomba Waziri wa Michezo, Mohamed Mchengerwa kusimamia kikamilifu katika uwekezaji hata wa makocha na walimu wa timu za michezo kama zinavyofanya timu zingine nchini.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz