Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge abanwa kwa kusahau kuitakia ushindi Simba

Simba X Yanga CAF Simba vs Yanga

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kiteto (CCM), Edward Ole Lekaita amezua kizaazaa bungeni baada ya kuitakia heri Klabu ya Yanga pekee inayocheza mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns na kuisahau Simba na hivyo kuhojiwa na Spika kuhusu dhana ya uzalendo katika michuano ya kimataifa.

Hayo yamejiri leo ljumaa Aprili 5, 2024 wakati mbunge huyo akichangia mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya VWaziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Baada ya Spika Dk Tulia Ackson kumkumbusha kuhusu uzalendo, Lekaita alizitakia klabu za Simba na Yanga mchezo mwema na akizitaka ziibuke na ushindi dhidi ya wapinzani wao ili zifuzu kwenda hatua ya nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live