Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazili wa Simba ataka kufunga mabao 10 au 15

78313 Mbrazil+pic

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji mpya wa Simba, Mbrazili Wilker Da Silva amesema akipewa nafasi zaidi ya kucheza anaweza kumaliza msimu huu akiwa amefunga mabao kati ya 10 mpaka 15.

Da Silva aliichezea Simba kwa mara kwanza tangu alipojiunga nayo baada ya kuingia akitokea benchi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Da Silva, alisema haikuwa kazi rahisi kupata nafasi ya kuitumikia timu hiyo kwani kuna wachezaji wengi wenye uwezo ambao wanafanya vizuri katika nafasi ya ushambuliaji.

"Nilikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, lakini kurudi tu uwanjani kocha Patrick Aussems amenipa nafasi ya kutumika ingawa si dakika nyingi huu ni mwanzo, lakini kadri muda ambavyo unazidi kwenda naimani nitatumika zaidi," alisema.

"Nipo tayari kwa kushindana kutokumungusha Aussems, ambaye atakuwa ananipa nafasi ya kucheza kwani kufanya hivyo nitaweza kuisaidia timu na kufikia malengo yake ya kutetea ubingwa msimu huu.

"Sijafunga bao hata moja, lakini nimejiwekea malengo ya kufikisha 10 mpaka 15, kama nikiwa mzima jambo ambalo naimani kwa kushirikina na wachezaji wenzangu.”

Pia Soma

Advertisement
“Ushindani wa namba ndani ya timu ni mkubwa haswa katika nafasi ya ushambulia wote ambao wanacheza hapo wanafanya vizuru kwa sasa," alisema Da Silva. 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz