Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazil wa Singida BS aionya Yanga

Bruno Gomes Mbrazili, Bruno Gomes

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Singida Big Stars (SBS) tayari kipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Mkapa ukiwa ni wa kwanza kwao kukutana msimu huu.

Mbrazili, Bruno Gomes ameweka wazi ugumu ambao watakutana nao; “Ni ngumu kucheza na bingwa mtetezi (Yanga) ingawa haitufanyi kuingia kwa kuwahofia, tunawaheshimu sana kwa sababu ya wachezaji wazuri waliyonao japo hata sisi ni bora kama walivyo wao pia.”

“Mchezo wetu uliopita na Simba ulitupa mwanga na jinsi ya kukabiliana na presha pindi tunapocheza na aina ya timu kubwa hivyo kwetu ilikuwa ni somo japokuwa tulicheza uwanja wa nyumbani tofauti na Yanga ambapo tuko ugenini.”

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Mathias Lule alisema tangu wamefika jijini hapa hali ya kikosi chake ni nzuri na kila mchezaji yuko tayari kwa ajili ya kupambania pointi tatu katika mchezo huo.

Katika kikosi hicho Bruno ndiye anayeongoza kwa kupachika mabao akiwa amefunga mabao matatu kwenye michezo 10 aliyocheza.

Kwenye michezo 10 iliyocheza Singida imeshinda mitano, sare tatu na kufungwa miwili ikiwa nafasi ya nne na pointi 18 wakati Yanga iliyocheza tisa imeshinda saba na droo mbili ikisalia kileleni na pointi zake 23.

Kwa upande wa kocha wa Singa, Hans Pluijm alisema anatambua wana mchezo mgumu dhidi ya Yanga lakini amekiandaa kikosi chake vya kutosha na anakuja kucheza soka la kuvutia huku wakisaka matokeo.

Pluijm alisema anajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote lakini hilo limetokana na ubora wa Ligi jinsi ulivyo hivyo inabidi uwasome wapinzani wako mara kwa mara.

“Mechi yao ya kimataifa hadi hii na Kagera kuna vitu ambavyo nimeviona vimebadilika na nitavifanyia kazi, walivyocheza huko inawezekana wasicheze sawa na sisi na hilo hata Simba ilivyocheza na sisi ni tofauti.”

Chanzo: Mwanaspoti