Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazil asepa Singida Big Stars, Kocha afunguka

Hans De Pluijm Mbrazil asepa Singida Big Stars, Kocha afunguka

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Timu ya Singida Big Stars, Hans Van Der Pluijm ametaja Sababu za Kutoonekana kwa wachezaji wa Kimataifa wanaokipiga Kunako Kikosi Hicho katika Michezo kadhaa ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Singida kuelekea katika mchezo dhidi ya wapinzani wao Coastal Union utakaochezwa kesho katika dimba la Liti.

Pluijm mesema miongoni mwa sababu za kutoonekana kwa baadhi ya wachezaji ni majeruhi, huku mchezaji mmoja kuomba kuondoka kunako Kikosi hicho.

Mchezaji ambaye ameomba Kuondoka kunako Kikosi Hicho kutokana na kile kilichotajwa ni kushughulikia masuala ya Kifamilia ni Peterson Cruz ambaye tayari alianza kuonyesha cheche kunako michezo ya Ligi Kuu.

Amesema wachezaji wengine ambao hawakuonekana Uwanjani kama Bruno na Dario ni kutokana na maradhi pamoja na majeruhi lakini tayari wapo fiti kuwavaa wagosi wa kaya Kesho.

Katika mazungumzo yake Kocha Hans Van Der Pluijm hata hivyo amedokeza juu ya mipango ya Timu hiyo katika usajili akisema wamejitayarisha kuipa uimara zaidi Timu hiyo kwa Kusajili wachezaji wenye ushindani katika Mashindano ya Kimataifa.

Aidha Kocha Huyo amesema Maandalizi Kuelekea katika mchezo wa kesho yamekamilika na wachezaji wapo katika morali nzuri tayari kuvuna alama dhidi ya Wagosi wa Kaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live