Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbongo aula 'pre-season' Hull City

Mbongoo Mshambuliaji kinda wa Kitanzania, Jack Topley

Sat, 13 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji kinda wa Kitanzania, Jack Topley (16) amepata shavu la kwenda Uturuki akiwa na kikosi cha kwanza cha Hull City kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza England ambalo ni maarufu kama Championship.

Kocha wa Hull City, Tim Walter ameamua kutoa nafasi hiyo kwa Mtanzania huyo pamoja na vijana wengine wa ngazi tofauti za vijana ili kupigania nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao.

Katika kambi hiyo ya awali, mbali na wachezaji vijana, Walter ameenda na wachezaji 19 wazoefu ikiwemo wapya ambao wamesajiliwa katika dirisha hili la usajili kama vile Julian Hubner, Filip Tapalovic na Erbil Bozkurt.

Akiongelea fursa hiyo, Jack alisema yupo tayari kujaribu bahati yake kama ilivyokuwa kwa kinda mwenzake, Lamine Yamal aliyepenya kutoka akademi ya Barcelona iitwayo La Masia hadi kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

"Kikubwa ni kuonyesha tu mengine ni kumwachia mwalimu nadhani yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho, nipo tayari kujaribu bahati yangu, ninafuraha kuwa sehemu ya maandalizi ya msimu ujao nikiwa na kikosi cha kwanza," alisema.

Jack amekuwa sehemu ya kikosi cha Hull City chini ya miaka 18 na amekuwa miongoni mwa vijana ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika ngazi hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti