Straika mwili jumba wa Simba Sports Club, Chriss Mugalu yuko fiti kuweza kuipambania Simba katika harakati zake za kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.
Mugalu ambae alikuwa nje kwa miezi kadhaa kutokana na majeruhi amepona na sasa ni suala la Mwalimu tu kuamua amtumie wapi na lini.
Katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Simba Sports, wameandika taarifa ya kumkaribisha kwa mara nyingine straika huyo kikosini.
"Anarudi uwanjani kutupa furaha" imesomeka sehemu ya taarifa hiyo
Mwalimu aliepita wa Simba, Didier Gomes Da Rosa alipenda kumtumia Mugalu dhidi ya Bocco na Meddie Kagere, sasa hivi Simba kuna mwalimu mpya haijajulikana bado atapewa kipaumbele ama la!.
Mugalu aliumia mwanzoni mwa msimu huu katika mechi dhidi ya Biashara United ya Mara.