Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbona patachimbika wikiendi hii

Mbao Fc Players  Mwassa  Captain   Said Khamis  Top Scorer   Pastory Athanasi And Evarigestus Mujwah Mbona patachimbika wikiendi hii

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By YOHANA CHALLE LIGI Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea tena wikiendi hii mzunguko wa tatu, huku mchezo wa kukatana shoka utakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC ikiikaribisha Pamba FC.

Utakuwa mchezo wa kukatana shoka kwenye dabi hiyo kutokana na timu kufahamiana vyema kutoka mkoani Mwanza na kuwavutia watazamaji wengi wa mkoa huo.

Mchezo mwingine wa wikiendi hii, Fountain Gate itacheza na Transit Camp zote zikiwa zimeshinda michezo yake yote miwili, Singida United itakipiga na Kitayosce Uwanja wa Liti, Singida.

AFC ikicheza na Rhino Rangers huku Alliance ikimalizana na Geita Gold. Kundi A kinara wa kundi hilo African Sports ikikipiga na Boma FC, Gipco na African Lyon, Lipuli FC na Mbeya Kwanza.

Ndanda FC ikirejea nyumbani kwa mara ya kwanza itaikaribisha Njombe Mji wakati Majimaji itafunga wiki kwa kucheza na Mawenzi Market.

Kocha wa African Sports, Musa Six alisema lengo lao ni kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo kwenye kundi hilo na kuzidi kuwa na matumaini ya kupanda Ligi Kuu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz