Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbombo nje wiki tatu

Mbombo Idris.jpeg Idris Mbombo

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Azam FC, Idris Mbombo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu baada ya kusumbuliwa na jeraha la goti.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam daktari wa timu hiyo, Mbaruku Mlinga alisema nyota huyo alianza kusikia maumivu katika mchezo na Mashujaa uliopigwa Novemba Mosi mkoani Kigoma ingawa ilionekana sio siriasi kama ilivyo sasa.

“Baada ya hapo aliendelea vizuri na programu za mazoezi na wachezaji wenzake ila alijitonesha tena sehemu ya goti lake wakati wa mchezo na Ihefu kule Mbeya hivyo tulimfanyia vipimo na kugundua ni jeraha ambalo ni siriasi kidogo,” alisema.

Mlinga aliongeza baada ya vipimo vya awali imegundulika atakuwa nje kwa wiki tatu huku akiwa kwenye uangalizi mzuri wa madaktari.

Kwa upande wa kocha mkuu wa kikosi hicho, Youssouph Dabo alisema ni bahati mbaya kwao na kwa nyota huyo kwani wao kama benchi la ufundi hufurahia kuona wakiwa na wachezaji wote hasa katika kipindi hiki ambacho wana michezo mingi muhimu.

“Kila kocha anapenda kuona akiwa na wachezaji wake bora kikosini kwa sababu inatoa wigo mpana wa machaguo kutokana na aina ya mpinzani tunayekutana naye, ni bahati mbaya kwake lakini ni nafasi kwa wengine kuonyesha ubora waliokuwa nao.”

Chanzo: Mwanaspoti