Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbombo na mipango ya Ubingwa, amtaja Kessy

Mbomboo Mshambuliaji wa Azam FC, Idriss Mbombo

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mshambuliaji wa Azam FC, Idriss Mbombo amesema wana nafasi kubwa ya kutwaa taji la msimu wa 2021/22 kutokana na usajili uliofanywa na uongozi wao.

Mbombo amesema wachezaji wengi wanafahamiana na baadhi wamefundishwa na kocha George Lwandamina, hivyo kilichobaki ni utekelezaji.

“Nimefundishwa na Lwandamina, nimecheza na Rodgers Kola, Paul Katema, Charles Zulu na Prince Dube. Pia ukiachana na kuwafahamu vizuri nyota hao kwa muda mfupi niliokaa nao nimeona tuna kikosi bora, tushindwe sisi tu kutwaa taji la ligi,” amesisitiza nyota huyo.

“Unacheza timu ambayo nyota zaidi ya saba wameitwa vikosi vyao vya taifa, hili tu linaonyesha kuna timu nzuri tukiunganisha nguvu wachezaji, viongozi na mashabiki tuna uwezo wa kutwaa taji”.

Mbombo amesema anafahamu mifumo ya Lwandamina na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ndani ya muda aliofika na kufanya mazoezi pamoja anaiona timu hiyo mbali kwenye mashindano ya kimataifa.

“Nipo tayari kujitoa kwa nguvu zote lengo kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara. Nina imani Lwandamina ataifikisha mbali timu kwani ina mazingira mazuri kwa wachezaji, kilichopo ni kuwathibitishia hawakukosea kutupa nafasi.”

Wakati huohuo Mbombo alimtaja Hassan Kessy kuwa ni moja ya walinzi bora wa kulia aliowahi kucheza nao akitoa sifa za beki huyo kuwa anajua afanye nini wakati gani.

“Kuna mechi moja ilikuwa ngumu sana, akanifuata ikiwa imebaki dakika moja akaniambia nahodha kaa pale kati mimi naleta mpira tunashinda, kweli bana kapata mpira kapiga cross palepale nilipo nikapiga kichwa goli, namheshimu sana,” amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz