Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbivu na mbichi kesi ya Morrison CAS

Brnarrd Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa leo ni August 24, 2021, siku ambayo kesi inayomkabili mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison katika mahakama ya usuluhishi ya Michezo CAS,itatolewa hukumu.

Shauri hilo linawahusu Yanga wanaodai kuwa bado walikua na mkataba na mchezaji huyo wakati akisaini kwa watani wao Simba SC. Hivyo alikua ni mchezaji wao halali.

Kesi hiyo ilipangwa kutolewa uamuzi kati ya tarehe 4 Agosti mpaka 24 Agosti na si zaidi ya hapo.

Kwa Upande wao Klabu ya Yanga wamesema tarehe hiyo ilitolewa na CAS wenyewe na kwa kuwa siku inaisha saa sita usiku hivyo wanavuta subira kuona ni maamuzi gani yatakayotolewa.

Bernard Morrison yuko nchini Morocco na Klabu yake anayoichezea hivi sasa Simba SC ambako ndiko walipoweka kambi wakijifua kujiandaa na msimu mpya wa 2021/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live