Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbinu za gamondi vs Dabo zilivyoumana kwa Mkapa

Aziz Sillah Mbinu za gamondi vs Dabo zilivyoumana kwa Mkapa

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC dhidi ya Azam Fc ilikuwa mechi yenye hadhi ya Ligi Kuu, tumeona kila kitu kuanzia kasi, ufundi, mpambano haswa, kujituma na magoli.

Namna ambavyo Kocha Miguel Gamondi wa Yanga anavyowatumia Maxi Nzengeli, Pacome na Aziz Ki katikati ya mstari wa kiungo na ulinzi wa timu pinzani ni kazi ngumu sana kwa wapinzani (between the lines).

1. Viungo hawajui kama wanatakiwa kushuka chini

2. Walinzi hawajui kama wanatakiwa kukabia juu

Kwa sababu Joyce Lomalisa anakuwa anasogea juu maana yake Yanga wanatengeneza "Box Midfield" kwa kuwa Job anabaki nyuma na Yanga kutengeneza umbo la 3-2-2-3 (Aucho na Muda + Aziz Ki na Pacome / Maxi mmoja wapo akienda pembeni) maana yake Yanga wanakuwa na fursa kubwa ya kucheza ndani huku wakijua pembeni wana spare man ( Lomalisa).

Azam FC dakika 10 za kwanza walikuwa wanapata tabu kuwafungua Yanga hasa kufika phase ya pili kwa nini ?

1. Yanga walikuwa wanazuia kwa 4-1-4-1 (Aucho peke yake kwenye 6 na mbele yake mstari wa wachezaji wanne)

2. Azam FC kwenye build walikuwa na namba 8 wawili Fei Toto na Akaminko pembeni ya Aucho, shida yake ni Bajana hakuwa anapata nafasi au njia ya kupiga pasi nyuma ya mstari wa wachezaji wanne wa Yanga.

3. Baadaye Kocha Dabo alibadilisha na Azam wakaanza kucheza soka safi sana, Akaminko akashuka kuwa na Bajana maana yake Fei Toto akabaki namba 10 na alikuwa anaombea mpira maeneo ya hatari sana dhidi ya Aucho.

Kuna nyakati timu zote mbili zilikuwa na ugonjwa huu: "Ukishambulia haraka upo hatarini kushambuliwa haraka" walikuwa wanalazimisha kwenda mbele haraka matokeo yake "Turn Overs" zinatokea zenye hatari.

1. Sillah kacheza mechi nzuri sana, alilazimisha Bacca awe anatoka kati kwenda kumsaidia Lomalisa.

2. Lusajo, haimbwi sana lakini kwenye kuzuia anawapa Azam uimara sana

3. Iddrisu saves nzuri na then kosa moja, adhabu

4. Maxi ni elusive, ngumu sana kukabiliana naye, yupo busy mno

5. Pacome technical ability.

6. Mzize anahitajika kuboresha haraka , movement sawa lakini vilivyobaki aboreshe.

7. Aziz KI alikuwa na mechi nzuri, nguvu kubwa mguuni na maamuzi sahihi ya kupiga mashuti mwisho wa siku akaondoka na mpira wa hat trick.

8: Azam FC kufungwa 3-2 nafuu kwao ingekuwa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live