Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbinu tano za kuibeba Yanga

79858 Yanga+pic

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MASHABIKI wa Yanga wana kila sababu ya kufurahia baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuirahisishia timu yao baada ya kuwajulisha wanaweza kuwatumia nyota wake David Molinga na Moustafa Seleman dhidi ya Pyramids ya Misri.

Yanga itaavana na Pyramids katika mechi ya ‘play-off’ ya Kombe la Shirikisho Afrika ikianzia nyumbani mwishoni mwa Oktoba, kisha kurudiana nao wiki moja baadaye nchini Misri na mshindi wa jumla kutinga makundi ya michuano hiyo.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba kwenye mchezo huo, Yanga huenda ikawatumia wachezaji hao baada ya kufahamishwa vibali vya vyao vipo katika hatua ya mwisho kutolewa, baada ya awali kuiandikia CAF barua ya kuwaombea leseni zao.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema uongozi uliiandikia barua CAF wiki iliyopita kuwakumbushia ombi lao la leseni za wachezaji hao, ambapo mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodger Gumbo alithibitisha wamefahamishwa kila kitu kipo sawa lakini bado hawajatumiwa leseni hizo.

Yanga inawahitaji wachezaji hao kutokana na ugumu wa mchezo huo na pia taarifa za kuumia kwa Kelvin Yondani kwenye beki ya kati, huku Molinga akiwa ameanza kung’ara kwa kufunga

mabao

Pia Soma

Advertisement
katika mechi za timu hiyo.Molinga amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara na mengine matatu katika mechi za kirafiki hivi karibuni.

“Unawezaje kuwakosa wachezaji hao katika mechi hizo mbili. Benchi la ufundi limeliona suala hilo na kutuletea kulifanyia kazi. Tumeandika barua CAF tokea wiki iliyopita kuomba kupata leseni zao,” alisema Mwakalebela.

Hata hivyo mchana wa jana Gumbo alisisitiza CAF imewapa majibu suala hilo lipo hatua ya mwisho na itawatumia wachezaji hao kwani watatumiwa leseni za nyota hao kabla ya mechi ya kwanza itakayochezwa Oktoba 27. “Tumehakikishiwa na CAF kwamba kila kitu kipo vizuri, bado kutuma tu kwa sababu awali tulichelewa usajili wa mechi za awali, lakini kwa hatua hii ya playoff na hata makundi hawazuiliki tena, hii ni taarifa nzuri kwetu,” alisema Gumbo.

Katika msisitizo juu ya mchezo huo na Waarabu, Mwakalebela alisema: “Tuna mikakati yetu, hivyo hatuhitaji kupata visingizio, tumeanza kujiandaa vilivyo na benchi la ufundi limeanza kufanyia kazi mechi hiyo, si mechi rahisi, ina hadhi yake ya ugumu, lakini mikakati yetu ni kushinda.”

Katika kuwaweka vyema wachezaji wao ambao hawajaitwa timu za taifa, Yanga asubuhi ya leo itavaana na Friends Rangers kwenye viwanja vya Gymkhana kabla ya Oktoba 16 kucheza mchezo wa mwingine wa kirafiki dhidi ya Pan Africans.

Chanzo: mwananchi.co.tz