Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbinu mpya ya Zahera Yanga hii hapa

MWINYI ZAHERA?fit=1280%2C720&ssl=1 Mbinu mpya ya Zahera Yanga hii hapa

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BOSI wa Maendeleo Soka la Vijana Yanga, Mwinyi Zahera amesema amefurahishwa na vipaji vilivyopo na kuahidi kuviendeleza kwa manufaa yao na atasuka upya na kuboresha vitu vingi.

Akizungumzia wachezaji hao alioanza nao mazoezi rasmi Jijini Dar es Salaam, Zahera alisema mwanzo wakati wanaanza maandalizi walikuwa na shida ila kumekuwa na maboresho makubwa tangu alipochukua kikosi hicho.

“Wachezaji wengi walikuwa na shida kwa sababu nilikuwa nawaambia wakimbie mita 800, kwa dakika nne lakini wengi wao walikuwa wanashindwa ila kwa sasa kumekuwa na maendeleo mazuri,” alisema.

Aliongeza kwa sasa anazingatia uimara kwa wachezaji pamoja na mbinu za kiufundi kitu ambacho ni muhimu kwa mtoto anayecheza soka la akademi.

“Huu ni mwanzo tu ila naamini mpaka kufikia mwezi ujao nadhani watakuwa bora zaidi ya hapa walipo kwa sasa, lengo ni kuwajengea uwezo wa kufikiri na kuwapa nafasi ya kufika mbali,” alisema.

Mchezaji na Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni alisema msingi wa soka huanzia kwa vijana hivyo kuna kila sababu na umuhimu wa kuwaandaa wachezaji hao kwa manufaa ya kizazi kijacho.

“Timu zilizoendelea zimewekeza huko hivyo ni jambo jema kuona timu zetu zikiwekeza kwao na kufundishwa na makocha wakubwa, ni wakati wa kuwapa nguvu na sapoti,” alisema.

Zahera amereja Yanga baada ya hapo awali kuitumikia timu hiyo akiwa Kocha Mkuu na kuwa miongoni mwa makocha wakubwa wanaofundisha soka la vijana.Mohamed Badru aliyetoka Mtibwa Sugar amepewa timu ya vijana ya Azam FC.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz