Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya city kusaka Vipaji kwa ajili ya Msimu ujao

Kibu Dennis?fit=1920%2C1080&ssl=1 Kibu Denis

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wakati ikielezwa kuwa tayari Kibu Dennis amemalizana na Simba kwa ajili ya msimu ujao, Uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kwamba kwa sasa upo chimbo kusaka wachezaji wapya.

Imeelezwa kuwa kwa sasa Kibu yupo Dar kwa lengo la kumalizana na mabingwa wa Tanzania Simba ambao walimpeke ghym kujiweka fiti.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Mathias Rwambiza alisema kuwa hesabu kubwa ni kusajili wachezaji wazuri ili kuziba nafasi kwa ajili ya wale ambao wataondoka.

“Ikiwa kuna mchezaji ataondoka basi tutafanya kazi kubwa ya kuweza kumtafuta mbadala wake kwa kuwa hatuwezi kuwazuia wachezaji wetu ambao watahitajika na timu nyingine haitupi tabu.

“Wale watakaoondoka basi kazi itakuwa ni kumtafuta mbadala wake kikubwa ni kuona kwamba timu haiypi wala kupoteza ramani,” alisema.

Chanzo: globalpublishers.co.tz