Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Kwanza yapiga panga tisa

Mbeya Kwanza Watu 9 Mbeya Kwanza yapiga panga tisa

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuanza kwa kishindo akiiongoza Mbeya Kwanza kushinda mechi mbili mfululizo, Kocha mkuu wa timu hiyo, Michael Mnyali, ametangaza kutembeza ‘fagio’ kikosini kwa kuwatema nyota tisa na kuingiza sura mpya tano.

Mnyali alijiunga na timu hiyo hivi karibuni baada ya kutemwa Ken Gold na alianza mechi ya kwanza dhidi ya Cosmopolitan kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho na kushinda kwa penalti 4-3, baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu.

Juzi Jumapili kocha huyo akiwa pamoja na Stepehen Matata ambao wana rekodi ya kuipandisha timu hiyo ligi kuu, waliiongoza kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Pan African kwenye Uwanja Uhuru Dar es Salaam na kusogea hadi nafasi ya nne kwa pointi 24.

Mnyali alisema licha ya matokeo mazuri aliyoanza nayo, lakini kutokana na malengo ya timu hiyo hana budi kufanya mabadiliko kwa kuwapunguza baadhi ya wachezaji ambao anaona kasi yake imewashinda.

Alisema kwenye dirisha dogo anahitaji kuongeza nyota watano katika nafasi ya beki wa kati na wa kushoto, winga na kiungo na wote lazima wawe na uwezo mkubwa ili kuziba mapengo ya wenzao tisa watakaoachwa.

“Kuna ambao ni majeruhi wengine kasi imekuwa ndogo, hivyo lazima tufanye mabadiliko tuongeze nguvu, nikipata wazoefu itapendeza japokuwa nalenga sana wenye uwezo siyo mtu anakuja tu,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti