Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Kwanza ndo hivyo tena

Mbeya Kwanza Watu 9 Mbeya Kwanza ndo hivyo tena

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Mbeya Kwanza ikijiandaa na mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Pan African, benchi la ufundi limekiri kuwa msimu huu kupanda imekuwa ngumu badala yake mipango inaanza upya kwa ajili ya msimu ujao.

Mbeya Kwanza ambayo ilishuka msimu uliopita, kwa sasa ipo nafasi ya nane kwa pointi 36 na hesabu za kumaliza ‘top four’ au kuwania kurejea ligi kuu zimeshakwama.

Meneja wa timu hiyo, David Naftar alisema kwa sasa hesabu zao zimeshakwama kuwania kupanda daraja, hivyo wanatarajia kuanza mapema maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.

Alisema timu ilikuwa na kikosi bora lakini zipo sababu kadhaa zikiwamo za wapinzani wao kuwazidi mipango nje ya uwanja hivyo wanaenda kurekebisha mapungufu na kuja upya msimu ujao.

“Msimu huu naona haiwezekani tena kuwania kupanda ligi kuu, tulikwama mapema kimipango hivyo tutapambana msimu ujao kuweka mazingira mazuri ili kufikia malengo,” alisema Naftar.

Alisema pamoja na kutofikia ndoto yao, lakini wanashukuru timu haipo nafasi mbaya ya kushuka daraja akibainisha kuwa hata mechi zilizobaki wanahitaji ushindi.

Timu hiyo imebakiza mechi tatu ikiwa ni dhidi ya Pan African, Biashara United na Copco ambazo zote itacheza nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea

Chanzo: Mwanaspoti