Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Kwanza kuachana na wachezaji 16

Dc041bec6f18550d4e5c9b58e9784966.jpeg Mbeya Kwanza Football Club

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza Maka Mwalwisi amesema timu yake itaachana na wachezaji 16 katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Akizungumza na gazeti hili jana Mwalwisi alisema kati ya hao wapo watakaopelekwa kwa mkopo kwingine na wengine wataachana nao kutokana na kushindwa kuonesha kiwango kinachohitajika.

‘’Tumekuwa na wachezaji wengi ambao tumeona tuwatoe kwa mkopo ili waweze kwenda kusaidia katika klabu nyingine na kuonesha kile ambacho wanacho, Pia, tutasajili kwa kuzingatia mahitaji yetu na katika nafasi zipi’’ alisema Mwalwisi.

Alisema timu yake itasajili golikipa mmoja, beki wa kati mmoja na mshambuliaji mmoja.

Mwalwisi alisema mpaka sasa kwenye kikosi chao wamefanikiwa kuongeza baadhi ya wachezaji akiwemo Habibu Kiyombo (Mchezaji huru), Yusuph Abas (Coastal Union) na Abdul Hamis (Coastal Union).

Alisema wacheza waliowatoa kwa mkopo na kuwapelekea timu ya Ken gold ni wawili ambao ni Peter Mwaisana na Ramadhan Kimata.

Akielezea kuhusu Ligi Kuu, Mwalwisi alisema ligi imekuwa ngumu sana kutokana na kila timu inaonyesha upinzani na kwamba wataendelea kupambana kufanya vyema katika ligi hiyo.

Katika msimamo wa ligi kuu, Mbeya Kwanza ipo katika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza michezo 11 mpaka sasa.

Timu hiyo imeshinda mechi mbili,sare tano na imepoteza michezo minne.Mbeya Kwanza imefunga mabao 11 na kufungwa mabao 13. Mbeya Kwanza inatarajia kucheza mchezo ujao wa ligi kuu na Azam FC Januari 16 katika uwanja wa kumbukumu ya Sokoine.

Chanzo: www.habarileo.co.tz