Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Kwanza, Dodoma Jiji hakuna mbabe

Kwanza Full Pic Data Mchezo wa Mbeya kwanza dhidi ya Dodoma Jiji

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mpira wa nguvu. Ndivyo unaweza kuelezea mchezo baina ya Mbeya Kwanza na Dodoma Jiji jinsi ulivyokuwa wa kasi na matukio ya hapa na pale.

Katika mchezo huo ambao umepigwa dimba la Sokoine jijini hapa, kila timu ilionesha uwezo wake kusaka ushindi huku nguvu na kasi ikiwa ni baadhi ya vitu vilivyochagiza mechi hiyo kuwa na mvuto.

Hata hivyo Dodoma Jiji watajilaumu kutokana na nafasi zaidi ya mbili zolizokuwa za wazi ambazo pengine zingeweza kuwarudisha jijini Dodoma kifua mbele.

Katika mchezo huo, Mbeya Kwanza ambao ndio msimu wao wa kwanza katika Ligi Kuu, walionesha nidhamu baada ya kucheza pungufu.

Mbeya Kwanza walicheza pungufu kuanzia dakika ya 26 baada ya beki wao wa kati, Joseph Majagi kuoneshwa kadi nyekundu na kuifanya timu hiyo kucheza kwa tahadhari zaidi.

Hata hivyo, katika mechi hiyo ilishuhudiwa rafu za hapa na pale, huku baadhi ya wachezaji wakimaliza na bandeji kichwani, akiwamo Paul Peter wa Mbeya Kwanza.

Kwa matokeo hayo, Mbeya Kwanza wanafikisha pointi tano huku Dodoma Jiji wakifikisha alama nne baada ya mechi tatu kila timu.

Kocha Mkuu wa Mbeya Kwanza, Hererimana Haruna amesema kadi nyekundu ndio iliwaharibia mipango na kwamba pointi moja si haba.

"Ligi ni ngumu, hakuna mechi nyepesi, kadi nyekundu ilitutoa mchezoni kwani tuliamua kurudi nyuma kucheza kwa tahadhari" amesema Haruna.

Naye Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema walistahili kushinda mechi hiyo, lakini safu ya ushambuliaji ilikosa umakini kumalizia mipira ya mwisho na kuahidi kilifanyia kazi.

"Ushindani ni mkali, tunashukuru kwa pointi moj kwani kwa sasa kila timu imejizatiti kutokana na hali ya uchumi ilivyo, hakuna changamoto yoyote" amesema Makata.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz