Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Kwanza, Biashara United hakuna mbabe

Biashara Sare Biashara yaambulia sare na Mbeya Kwanza

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabadiliko waliyoyafanya Biashara United kumtoa kiungo, Ramadhan Chombo 'Redondo' ni kama yaliwapa nafasi kubwa Mbeya Kwanza kuutawala mchezo hasa kipindi cha pili na kujikuta wakisawazisha bao.

Katika mechi hiyo ambayo imepigwa leo Ijumaa, Oktoba 29 katika uwanja wa Sokoine jijini hapa, kipindi cha kwanza Biashara United walionesha soka safi na la nidhamu ukilinganisha na wapinzani.

Kutokana na ufundi wa kiungo wao mkongwe, Redondo alionekana kuipa utulivu timu lakini kuipa bao la mapema dakika ya 13 alipopiga shuti la umbali na kujaa wavuni lililodumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Redondo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Notikel Masasi lakini hatua hiyo ilionekana kuidhohofisha eneo la kiungo na kuwapa nafasi wenyeji kuutawala mchezo.

Dakika ya 79, Hamis Kanduru aliisawazishia bao Mbeya Kwanza lakini wakiipa misukosuko eneo la mabeki kutokana na mashambulizi ya hapa na pale na hadi dakika 90 kumalizika timu hizo zikaondoka kwa sare ya bao 1-1.

Kwa matokeo hayo Mbeya Kwanza wanafikisha pointi sita ikiwa ni sare ya pili mfululizo huku Biashara United wakifikisha alama tano baada ya timu zote kucheza mechi tano.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz