Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Derby , Sokoine hapatoshi leo

Mbeya Derby Prison Vs Ihefu Mbeya Derby , Sokoine hapatoshi leo

Sat, 21 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Bara itaendelea leo kwa michezo miwili, huku kazi ipo Uwanja wa Sokoine kwa Tanzania Prisons na Ihefu zilizopo kwenye janga la kushuka daraja.

Mechi hiyo itapigwa Saa 10:00 jioni huku kila timu ikiwa na kiu ya kupata pointi tatu ili kujinusuru kwenye nafasi walizopo, Prisons ipo nafasi ya 11 na pointi 21 wakati majirani zao, Ihefu kutoka Mbalali ipo nafasi ya 13 na pointi 20.

Mbali na mechi hiyo pia kuna pambano lityapigwa saa 1 usiku kwa wenyeji Kagera Sugar wenye pointi 24 katika nafasi ya nane itakayoialika Coastal Union, yenye pointi 18 ikiwa nafasi ya 14 kwenye Uwanja wa Kaitba, Bukoba.

Katika mechi ya Prisons na Ihefu zilizotoka sare ya 1-1 mechi ya duru la kwanza, wageni wanatarajiwa kuwa na sura mpya baada ya kuwasajili Wanigeria wawili, Victor Akpan na Nelson Okwa kwa mkopo kutokea Simba, MburkinaFaso, Yacouba Sogne kutoka Yanga, Rashid Juma na Hussein Masalanga waliokuwa Ruvu Shooting, Adam Adam kutokea Mtibwa Sugar, Yahya Mbegu kutoka Geita Gold na Mudathir Said kutoka Prisons ambao huenda wakaongeza ubora kikosini.

Prisons nayo ina majembe matano, akiwamo kipa Benedict Tinocco, Mohamed Ibrahim, Lambart Sabiyanka, Shaban Kisiga na Meshack Suleiman kutoka Nyassa Big Bullets ya Malawi.

Timu zote zimetoka kupoteza mechi zilizopita, Prisons ikifungwa 3-0 na Azam siku chache tyangu watunguliwe 7-1 na Simba, wakati Ihefu ikuitoka kulala 1-0 kwa Yanga siku chache ilipoinyoa KMC.

Makocha wa pande zote watamba kujipanga ili kupata matokeo mazuri ndani ya dakika 90, kocha Patrick Odhiambo wa Prisons alisema timu yake imekuwa na matokeo mabaya, ila itarudi kwenye ari ya ushindani kama ikiishinda Ihefu.

"Kuna ile hali ya ushindi imekosekana kikosini lakini tunataka kuitumia mechi na Ihefu kuirudisha na tumejipanga kushinda ili morali irejee," alisema Odhiambo, huku Zuberi Katwila wa Ihefu alisema kikosi chake kitakuwa na mabadiliko dhidi ya Prisons na lengo la kufanya hivyo ni timu ipate ushindi.

"Tutakavyocheza na Prison huenda ikawa tofauti kabisa kuanzia mbinu hadi wachezaji, na tumefanya hivyo kutokana na matakwa ya mchezo wenyewe ambao tunahitaji ushindi," alisema Katwila.

Kwa upande wa Kagera ambayo haijasajili dirisha dogo kocha Mecky Maxime alisema amekiandaa kiosi chake kucheza vizuri na kupata ushindi mbele ya Coastal Union.

"Tumetoka ugenini na kupoteza mechi mbili, sasa tupo nyumbani na tunameandaa timu ili kushinda mechi na Coastal na kurejesha morali kikosini," alisema Maxime, huku kaimu kocha mkuu wa Coastal, Joseph Lazaro alisema anatarajia vijana wake hawatamuangusha kwani amewaanda kucheza vizuri.

"Itakuwa mechi ngumu kwetu lakini naamini vijana wangu watapambana na kufanya kile tulichowaelekeza mazoezinmi na mwisho wa siku tupate matokeo tunayoyahitaji."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live