Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya Derby, Prisons waichapa Mbeya City

TZ Prisons Winner Kikosi cha Tz Prisons

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Mbeya City jana Disemba 25 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Prisons yamefungwa na Zabona Khamis dakika ya 27 na Samsons Mbangula dakika ya 47, wakati la Mbeya City limefungwa na Baraka Mwalubunju dakika ya 61.

Kwa ushindi huo, Prisons wanafikisha pointi 21 sawa na Mbeya City baada ya wote kucheza mechi 18, ingawa Maafande wa Jeshi la Magereza wanabaki nafasi ya 11 wakizidiwa wastani wa mabao na mahasimu wao hao wa mji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live