Klabu ya Mbeya City imepanda kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara kutoka nafasi ya 7 hadi ya 5 imefikisha alama 28. Wamepanda baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya leo April 28.
Mbeya City imepanda kwa nafasi mbili kutoka ya 5 hadi ya 7 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara
Bao pekee la mchezo huu la Mbeya City limefungwa na Joseph Ssemuju dakika ya 55. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Mbeya City baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo 7 iliyopita ya Ligi kuu ambapo walifungwa michezo 4 na sare 2. Kwa ushindi huu wamefikisha alama 28 wapo nafasi ya 5 katika michezo 21.
Kwa upande wa Biashara wamefungwa mchezo wa kwanza baada ya kucheza michezo 3 mfululizo iliyopita bila kupoteza. Wamesalia na alama 22 wakiwa nafasi ya 12 na wamefungwa mchezo wa pili mfululizo katika Dimba la Sokoine msimu uliopita katika uwanja huo walinyukwa mabao 4-0.
Ligi itaendelea tena kesho Aprili 29, 2022. Kwa mchezo mmoja ambapo Geita Gold FC watakuwa wenyeji wa Azam FC katika dimba la Nyankumbu Saa 10:00 Jioni.