Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City yaipoteza Namungo kimtindo

Dondoo Pic Mbeya City yaipoteza Namungo kimtindo

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mbeya City imemaliza kibabe dakika 90 kwa kuilaza Namungo mabao 2-1 na kuifanya timu hiyo kupanda nafasi nne za juu wakiwashusha nafasi moja wapinzani hao na hizi ni dondoo sita za mechi hiyo.

.Mchezo huo unakuwa wa tatu kwa Namungo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ikicheza bila kuonja ushindi wowote ikipoteza miwili na sare moja.

.Mbeya City ilikuwa mechi yake ya tano katika uwanja huo ambapo ameshinda miwili ikiwamo dhidi ya Polisi Tanzania 3-1, sare mbili na Prisons 2-2 na Ihefu 1-1 na kupoteza mmoja mbele ya Azam FC 1-0.

.Mabao ya leo yaliyofungwa na Reliant Lusajo (Namungo) yanamfanya kubaki kileleni kwa mabao sita licha ya timu yake kupoteza, huku Sixtus Sabilo wa Mbeya City akifikisha mabao matano na asisti tano na kuongoza kwenye kipengele hicho hadi sasa.

.Katika mechi ya mwisho kukutana timu hizo kwenye uwanja wa Sokoine msimu uliopita, zilitoka sare ya bao 1-1 ambapo leo City imeondoka na ushindi huo na kufikisha pointi 15 sawa na wapinzani hao walioshuka hadi nafasi ya tano kutokana na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.

.Pamoja na mechi ya leo kuwa na rafu nyingi, lakini hakuna kadi ya njano wala nyekundu iliyooneshwa kwa mchezaji yeyote hadi dakika 90.

.Namungo ndio walipata kona nyingi (tano) dhidi ya wenyeji waliopata moja japokuwa wao walipata mabao mengi yaliyolenga lango (manne) kwa mawili huku yaliyotoka nje yakiwa moja moja kila upande.

Wengine wanaokimbizana kwenye ufungaji mabao ni Moses Phiri, Simba (5), Feisal Salum, Yanga (4) sawa na Matheo Anthony wa KMC.

Chanzo: Mwanaspoti