Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City yaifuata Simba kibabe

Simba Mbeya Duh Simba vs Mbeya City

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtihani mzito uko kwa Mbeya City kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumanne Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, huku ikianza safari leo.

Katika mchezo wa mwisho Mbeya City ilichapwa mabao 6-1 na Azam FC wakati Simba ilishinda mabao 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Kiwango cha Mbeya City kimezidi kushuka tofauti na ilivyoanza msimu ilikuwa na matokeo mazuri lakini kwa sasa inachechemea katika michezo yake.

Katika michezo 10 ya mwisho kucheza haijashinda mchezo wowote zaidi ya kuambulia sare sita, mara ya mwisho ilipata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani kwa kuichapa Namungo FC Novemba 4. Upande wa Simba katika michezo 10, imeshinda michezo minane na sare mbili, ile ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine na sare kama hiyo dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha msaidizi wa kikosi hicho, Anthony Mwamlima alisema kila jambo linakuwa na mapito yake katika kutimiza lengo hasa kwenye soka.

“Kuwa na matokeo ya namna hii siyo mara ya kwanza na Mbeya City siyo timu ya kwanza, kikubwa ni kuzidi kuwapa morali vijana ili wacheze kwa kujituma.

“Lengo la timu ni kuhakikisha mwisho wa msimu tunakuwa kwenye nafasi nzuri ambayo kila mmoja ataifurahia bila kuangalia sasa tunapita kwenye magumu yepi,” alisema Mwamlima.

Aliongeza mzunguko wa pili unaanza huku dirisha la usajili la wachezaji likielekea ukingoni wakiamini watapata wachezaji watakaokwenda kuongeza nguvu.

Kikosi hicho kilitarajia kuondoka jana lakini hakikufanikiwa, katibu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe alieleza mipango yao ipo sawa na timu itaondoka leo Jumamosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live