Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City yaichapa Kagera Sugar, Singida United jahazi linazama

97966 Pic+mbeya+city Mbeya City yaichapa Kagera Sugar, Singida United jahazi linazama

Thu, 5 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabao wawili ya mshambuliaji Yusuph Mhilu hayakutosha kuisaidia Kagera Sugar kuepuka kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera. Mabao hayo yanamfanya Mhilu kufikisha mabao 11 akiwa nyuma kwa magoli matatu kwa kinara wa ufungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Meddie Kagere wa Simba mwenye magoli 14, kabla ya mchezo wake wa baadaye dhidi ya Azam. Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, wageni Mbeya City inayopigana kukwepa janga la kushuka daraja ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake Kelvin John aliyefunga magoli mawili katika dakika 1, 17, huku Mohamed Kapeta akifunga bao tatu dakika 57. Mhilu aliifungia Kagera bao katika dakika 25 na bao lake la pili alifunga kwa penalti katika dakika 90. Biashara United imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani Karume, Mara kwa kuichapa Tanzania Prisons kwa bao 1-0, shukrani kwa goli la Mpapi Nasibu alillofunga dakika 4. Ushindi huo unaifanya Biashara United kufikisha pointi 38, baada ya kucheza mechi 26, na kujiweka katika mazingira salama ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao. Nayo Mtibwa Sugar imelazimishwa sare 1-1 na Namungo. Kwenye Uwanja wa Liti, wenyeji Singida United safari yao ya kushuka daraja inazidi kushika kasi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Coastal Union. Katika mchezo huo bao pekee la Coastal Union lilifungwa na Mudathir Abdallah katika dakika 22 na kuwafanya mabingwa hao wa mwaka 1988  kufikisha pointi 42 na kupanda hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu. Singida United imeendelea kuburuza mkia ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 26, hivyo kujiweka katika mazingira magumu ya kubaki katika ligi hii ambayo msimu huu zinashuka timu nne na mbili zinacheza mtoano. Mvua yatibua mechi za Ligi Kuu Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali nchini leo zimesababisha michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuahirishwa kutoka na viwanja kujaa maji. Mechi baina ya Lipuli dhidi ya Ndanda FC iliyokuwa ichezwe leo kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa imeahirishwa kufuatia mvua kubwa kunyesha na uwanja huo kujaa maji. Mvua hizo pia zimetibua mechi nyingine kati ya Mwadui FC dhidi ya Polisi Tanzania iliyokuwa ichezwe kwenye Uwanja wa Mwadui Complex imeahirishwa baada ya mvua kubwa inayonyesha Shinyanga. Mchezo kati ya KMC vs JKT Tanzania   umeahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji. Hadi mchezo unavunjika ulikuwa umechezwa kwa dakika 11 pekee na hakuna timu iliyokuwa na bao.  Mechi hiyo sasa itaendelea kesho saa 3 asubuhi kwa dakika zilizobaki. Miundo mbinu ya viwanja vingi nchini imekuwa tatizo jambo linalosababisha kipindi cha mvua mechi nyingi kushindwa kufanyika kutokana na viwanja kujaa maji. Kutokana na hali hiyo timu hizo zitalazimika kucheza mechi zake kesho asubuhi au kusubiri kupangiwa tarehe nyingine na TFF.

Chanzo: mwananchi.co.tz