Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City yagomea vichapo Champioship

Mbeya City Kushuka Mbeya City yagomea vichapo Champioship

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kusota kwa muda mrefu bila ushindi, Mbeya City imesema kwa sasa vipigo vimetosha na kazi inaanza upya katika mchezo ujao dhidi ya Pamba Jiji ili kujinasua nafasi za chini.

Timu hiyo ambayo ilishuka daraja msimu uliopita licha ya kuanza vyema Championship msimu huu, lakini hali imeonekana kuwa ngumu kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Mara ya mwisho vijana hao wa jijini hapa kupata ushindi ilikuwa Oktoba 1, walipoilaza Ruvu Shooting kwa bao 1-0 na tangu hapo wamepigwa hadi kushuka katika nafasi ya 11 wakiwa na pointi 11.

Kwa sasa timu hiyo chini ya kocha mkuu, Salum Mayanga inajiandaa na mechi ijayo dhidi ya Pamba Jiji iliyo nafasi ya tatu na pointi 18 itakayopigwa kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Sokoine.

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Mathias Wandiba alisema hawakuwa na matokeo mazuri akielezea mechi za ugenini zimekuwa ngumu, lakini kwa sasa kazi inaenda kuanza upya.

Alisema anafahamu mechi hiyo itakuwa ngumu, lakini kutokana na maandalizi waliyofanya na morali ya wachezaji wanakwenda kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri. “Tumepoteza mechi nyingi lakini ndio mpira. Tumerudi nyumbani kuanza upya dhidi ya Pamba Jiji na tunafahamu ugumu na umuhimu wa mechi hiyo kuhakikisha tunashinda,” alisema.

Kwa upande wake straika wa timu hiyo, Evaligestus Mujwahuki alisema walipambana katika mechi zilizopita, lakini bahati haikuwa kwao kushinda akiahidi michezo inayofuata kufanya kweli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live