Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City yaanza kuiwinda Yanga

Mbeya City Kushuka Mbeya City yaanza kuiwinda Yanga

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati mashabiki wa Yanga jijini hapa wakijiandaa kuipokea timu hiyo kwa shangwe la ubingwa wa Ligi Kuu iliyotwaa mapema kabla msimu haujamalizika, mabosi wa Mbeya City wamesema hitaji lao kwa sasa ni pointi tatu kutoka kwa vigogo hao ili kuepuka kushuka daraja na hesabu zimeanza.

Yanga, imeshatwaa taji la ligi mapema likiwa la 29 kwao tangu 1965 baada ya kuifunga Dodoma Jiji kwa mabao 4-2 wikiendi iliyopita ikifikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote kati ya 15 zilizosaliwa kwenye ligi hiyo, huku ikiwa na michezo miwili mkononi jijini hapas.

Mechi ya kwanza itakuwa ni dhidi ya City iliyopangwa kupigwa Mei 24 na kisha kufunga msimu na Tanzania Prisons na kwa sasa wanachama na mashabiki wa Yanga wanaendelea na vikao vya ndani wakijadili mapokezi ya timu hiyo ikiwamo sherehe za kupokea kombe hilo la ubingwa.

Hata hivyo, wenyeji City wameanza hesabu za kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo huo dhidi ya Yanga kwa nahodha wa timu hiyo, Juma Shemvuni alisema kwa vile Yanga imeshatwaa taji wao (City) bado hali si shwari hivyo wamejiandaa kushinda mechi hiyo kujiondoa nafasi za chini.

Alisema kwa sasa wachezaji wana ari na morali haswa baada ya ushindi kwenye mechi iliyopita dhidi ya Geita Gold, lakini hata sapoti wanayopata kutoka kwa wadau na mashabiki wa timu hiyo.

"Ushindani ni mkali lakini kila mmoja ni kushinda mechi zake, hatuangalii wa nyuma yetu wala wa mbele isipokuwa tunapambana na mechi zetu zilizobaki tukianza na Yanga kuhakikisha tunashinda" alisema Shemvuni, huku Meneja wa timu hiyo, Mwagane Yeya alisema ushindi walioupata dhidi ya Geita Gold ugenini umeongeza kujiamini kikosini na kwamba benchi la ufundi na uongozi unaendelea kuweka mipango na mikakati kukusanya alama sita zilizobaki.

"Hatujawa na matokeo mazuri na hii ni kutokana na mambo ya mpira, timu inapambana wanaonesha ushindani na sisi tumejipanga ndani na nje ya uwanja kushinda mechi zote zilizobaki" alisema Yeya.

Chanzo: Mwanaspoti