Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City waichapa Polisi Tanzania 3-1

Mbeya City FC.jpeg Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia moja ya mabao yao katika mchezo wa leo

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Mbeya City wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Hassan Nassor dakika ya 50, Sixtus Sabilo dakika ya 64 na Tariq Seif dakika ya 73 baada ya Vitalis Mayanga kuanza kuifungia Polisi dakika ya 16.

Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya sita, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake zake mbili ikiendelea kushika mkia baada ya wote kucheza mechi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live