Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City ni shidaaa!

Mbeya+city+pic Mbeya City ni shidaaa!

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIPA ASSA UKIACHANA na msimu uliomalizika ambao Mbeya City ilinusurika kushuka daraja bado inaendelea kukumbana na changamoto katika Ligi Kuu Bara kwenye mechi nne ilizocheza na haijaambulia kitu mpaka sasa.

Msimu uliopita Mbeya City iliponea chupuchupu kushuka daraja baada ya kucheza mechi ya mtoano na Geita Gold katika Uwanja wa Sokoine jijini humo, ambapo ilishinda mabao 2-1.

Oktoba 3, timu hiyo inacheza dabi na Prisons ambayo ipo nafasi ya 11, ikiwa imeshinda mechi moja, sare moja na kupoteza mbili na hivyo inamiliki pointi nne, huku Mbeya City ikiwa inaburuzwa mkia.

Kutokana na mwenendo huo, wadau wa soka wametoa mitazamo yao - kubwa zaidi wakielezea jinsi ambavyo mfumo wa timu kushuka daraja ulivyo mgumu na kwamba timu inayoanza vibaya ni rahisi kurejea Ligi Daraja la Kwanza.

Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, Bakari Shime anasema kwa mfumo wa sasa ambapo zinashuka timu nne moja kwa moja na mbili kucheza mchujo ni hatari kwa Mbeya City kuwa kwenye alama nyekundu endapo itaendelea na matokeo hayo. “Ligi ya sasa ni biashara asubuhi jioni hesabu, ina maana kwamba ukijiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi inakuwa rahisi mechi za mwishoni kujua zitakufikisha wapi, tofauti na kujikwamua kushuka daraja,” anasema.

Staa wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel anasema Mbeya City inatakiwa kujitafakari mapema ili kuweka mambo sawa kabla ya kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz