Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City mahesabu ni mengi kuliko uhalisia

Mbeya City Kushuka Wachezaji wa kikosi cha Mbeya City

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuati matokeo yasiyoridhisha kwa Mbeya City, uongozi wa timu hiyo umesema tayari umeandaa mipango na mikakati ya kuhakikisha hawashuki daraja, huku ukiwaomba wadau kuendelea kuisapoti timu hiyo.

Pia umewataka wanaochukulia motisha zinazotolewa na baadhi ya wadau wakiwamo viongozi wa Serikali na siasa kutochukuliwa kisiasa badala yake waungane kwa pamoja kuipa nguvu timu ili kufikia malengo.

Tayari baadhi ya wadau wa soka jijini Mbeya akiwamo mbunge wa zamani wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyeahidi Sh 1 milioni kwa kila bao la ushindi katika mechi zilizobaki, huku wabunge wengine mkoani humo wakikabidhi Sh 3 milioni.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Joseph Mlundi alisema moja ya jitihada walizofanya ni kuwashirikisha wadau kuiunga mkono City na kuongeza hamasa kikosini kuhakikisha wanashinda mechi zote.

“Kwanza tuna vikao vya mara kwa mara kujadili mustakabali wa timu, lakini tumewashirikisha wadau na tunaendelea kuwakaribisha wengine kusapoti Mbeya City na hizi motisha zisichukuliwe kisiasa,”alisema

“Tunaenda kuanza na Kagera Sugar Jumapili, kisha tutashinda dhidi ya Geita Gold bada ya hapo tutamfunga Yanga nyumbani na wale KMC ni halali yetu, hatutaki presha ya play off,” alisema Mlundi.

Mbeya City haipo salama kwenye ligi kuu ikiwa na pointi 28 katika nafasi ya 13 na kuwafanya wadau na mashabiki kuwa na presha juu ya timu hiyo wakihisi huenda ikashuka daraja.Hadi sasa City imebakiza mechi nne na Jumapili hii itakuwa uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kukipiga na Kagera Sugar ikiwa na uhitaji wa pointi tatu ili kufufua matumaini ya kubaki salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live