Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City kiulaini Sokoine

Officialmbeyacityfc 20211206 31 Mbeya City wakishangilia goli dhidi ya Dodoma

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoza Ushuru wa Jiji la Mbeya, Timu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Hussein Masalanga dakika ya 42 na Paul Nonga dakika ya 88.

Kwa ushindi huo timu hiyo inafikisha pointi 14 na kupanda nafasi ya tatu, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake12 ikishukia nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live