Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City hasira Mtibwa

Mubiru Mbeya City Mbeya City hasira Mtibwa

Sat, 21 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Abdallah Mubiru amekubaliana na matokeo yaliyotokea juzi baada ya kufungwa mabao 3-2 na Simba, lakini akaitangazia vita Mtibwa Sugar watakayokutana nayo kesho katika mechi hiyo akisema hasira zote watazimalizia kwao.

Juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, City iliendeleza matokeo mabovu katika mechi ya 11 mfululizo kwa kikosi hicho bila ya kupata ushindi tangu iliposhinda 2-1 dhidi ya Namungo Novemba 4, mwaka jana.

Akizungumza kocha Mubiru alisema ni matokeo mabovu kwao lakini amewapongeza wachezaji wake kwa jitihada kubwa walizozionyesha kuanzia mwanzoni mwa mchezo huku akiweka wazi makosa binafsi ndiyo yamewaangusha.

“Wachezaji wangu wamepambana na kuonyesha ni jinsi gani walikuwa na shauku ya kupata matokeo chanya, tumeumia sote ila sio muda wa kuanza kuangalia nyuma na badala yake tunarudi kujipanga tena kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema.

Kwa upande wa nyota wa kikosi hicho, Richardson Ng’ondya ambaye aliifungia timu hiyo bao moja dhidi ya Simba juzi, alisema wamesikitishwa na matokeo waliyoyapata kwani walipambana kwa juhudi zote licha ya kukiri pia ubora wa mchezaji mmoja mmoja kwa wapinzani wao ulichangia matokeo hayo.

Chanzo: Mwanaspoti