Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City, Mbao ni vita ya mabao Ligi Kuu

98509 Mbao+pic Mbeya City, Mbao ni vita ya mabao Ligi Kuu

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Mbeya City ikivaana na Mbao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo, safu zao za ushambuliaji zimebeba matokeo ya mechi hiyo.

Mbao iko nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 wakati Mbeya City wanashika nafasi ya 18 kwa pointi 27.

Mbeya City leo inamtegemea mshambuliaji Peter Mapunda mwenye mabao manane na Mbao inajivunia Waziri Junior aliyefunga saba.

Mapunda anayeshika nafasi ya tano katika chati ya wafungaji bora ndiye mchezaji tegemo katika kikosi cha Mbeya City.

Mbeya City imekuwa na mwenendo sio mzuri kwenye ligi hiyo kwani katika michezo mitano ya hivi karibuni imeshinda mitatu na kupoteza miwili.

Ilishinda dhidi ya Lipuli mabao 2-0, iliichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kabla ya kuifunga Kagera Sugar 3-2, ilipoteza dhidi ya Biashara United na Mwadui kwa kipigo cha bao 1-0 katika kila mchezo.

Pia Soma

Advertisement
Kocha wa Mbeya City, Amri Said alisema amejiandaa vizuri kushinda mchezo huo na amewaandaa wachezaji kupata matokeo. “Tuko katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi hivyo lazima tupambane kuhakikisha mchezo dhidi ya Mbao tunashinda ili tusogee juu,”alisema Amri.

Kwa upande wa Mbao ina kazi kubwa leo ya kuwakabili washambuliaji wa Mbeya City wakiongozwa na Mapunda huku safu ya ulinzi ikionekana kupitika kirahisi.

Katika michezo mitano iliyopita ya hivi karibuni safu ya ulinzi ya Mbao imeruhusu mabao tisa jambo ambao linaweza kuwaweka katika wakati mgumu kama mabeki hawatacheza kwa nidhamu.

Timu hiyo katika mechi tano imefunga mabao manne hivyo kuonyesha licha ya kwamba inapitika kirahisi katika eneo la ulinzi pia haina safu nzuri ya ushambuliaji.

Kocha wa Mbao, Abdulmutic Haji alisema ratiba ni kikwazo kwao kwa kuwa wanakosa muda wa kufanya maandalizi ya kutosha.

Alisema ugumu wa ratiba hiyo hautoi nafasi ya kujiandaa kutoka mechi moja hadi nyingine ingawa mchezo wa leo amesema pointi tatu ni muhimu.

“Ratiba ya ligi ni tatizo mechi ziko karibu tumetoka kucheza na KMC (Jumamosi) tukasafiri jana (juzi) tumefika Mbeya usiku sana, leo (jana) tumefanya mazoezi na kesho (leo) tunacheza, je hayo makosa tunayafanyia kazi saa ngapi, lakini hii haina maana tutacheza kwa hofu,”alisema Haji.

Chanzo: mwananchi.co.tz