Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City, Kagera Sugar hakuna mbabe Sokoine

DBD9340F 26AB 46AA A513 A6F8637DAE44.jpeg Mbeya City ililazimishwa sare ya magoli 2-2

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Mbeya City wamelazimishwa sare ya 2-2 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Novema 17 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Kagera Sugar walitangulia kwa mabao ya Anuary Jabir dakika ya 18 na Mbaraka Yussuf dakika ya 48, kabla ya Mbeya City kuchomoa kwa mabao ya Tariq Seif dakika ya 61 na Hassan Mahmoud dakika ya 81.

Kwa sare hiyo, Mbeya City, inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar imefikisha pointi 12 katika mchezo wa 12 nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live