Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya City, Coastal hakuna mbabe...Sabilo hakamitiki

Mby City Vs Coastal.jpeg Mchezo ulikwenda sare ya magoli 2-2

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu za Mbeya City na Coastal Union zimetoshana nguvu baada ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu NBC uliochezwa kwenye uwanja Sokoine.

Mabao ya Greyson Gwalala dakika ya 12, Sixtus Sabilo dakika ya 24 na 66 na Hamad Majimengi dakika ya 56 yakitosha katika dakika 90 na hizi ni dondoo za mpambano huo.

Huo unakuwa mchezo wa sita mfululizo kwa Mbeya City kucheza bila kupoteza ikishinda mitatu na sare tatu, huku Coastal Union ikiwa ni mechi yake ya nne mfululizo bila kupoteza ikishinda miwili na sare mbili.

Mabao mawili ya Sixtus Sabilo wa Mbeya City yanamuweka kileleni katika orodha ya vinara wa mabao akifikisha saba, huku Hamad Majimengi akifikisha mawili na nyota hao wote wanaweka rekodi ya kufunga katika mechi mbili mfululizo.

Mchezo huo ulikuwa wa 11 kwa timu hizo kukutana kwenye Ligi Kuu ambapo City wameshinda nne na Coastal Union wakishinda mitatu na sare tatu, japokuwa msimu uliopita Wagosi walitakata nyumbani 3-2 na ugenini bao 1-0.

Jumla ya kadi tatu za njano zilitolewa na mwamuzi Isihaka Mwalila kutoka Dar es Salaam ambapo wachezaji wawili wa Coastal Union Joseph Zziwa na Mtenje Juma huku kwa City akiwa ni Tariq Seif.

Mbeya City walipata kona tano dhidi ya wapinzani wao waliopata mbili katika mchezo huo ambao umepigwa uwanja wa Sokoine ukiwa wa kiporo.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kubaki nafasi tano za juu kwa pointi 16 wakiwa wamecheza mechi 10 huku Wagosi wa Kaya wakibaki nafasi yao ya 11 kwa pointi 12 wakicheza michezo tisa.

Chanzo: Mwanaspoti