Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbelgiji Luc achukia Yanga kutolewa mapema Mapinduzi

91426 Pic+yanga Mbelgiji Luc achukia Yanga kutolewa mapema Mapinduzi

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar.Kocha mpya wa Yanga, Luc Eymael hajafurahishwa na timu yake kutolewa mapema katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi akisema hataki kuona timu inadharauliwa.

Eymael amesema kuwa bado hakuelewa kwanini Yanga haikupanga kikosi kamili hasa katika mchezo wa nusu fainali.

Kocha huyo Mbelgiji amesema alitegemea katika hatua ambayo timu ilifikia alitaka kuona kikosi kamili kikitumika na sio kujaribu lengo likiwa kulinda jina na heshima ya klabu.

Amesema hataki kuona Yanga inaidharau timu yoyote pinzani na kwamba kila mchezo kwao utakuwa na uzito mkubwa.

Hata hivyo, kocha huyo amesema yapo mambo ameyabaini kwa wachezaji aliowaona jana na sasa anataka kuzungumza nao kwanza.

Ameongeza atakutana rasmi na wachezaji wake mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam leo tayari kwa kuanza mikakati ya kuanza kazi kwa kasi katika ajira yake mpya hiyo.

Shabiki wa Yanga, Ibadi Likungwa amesema hakufurahishwa hatua ya timu yake kutolewa na Mtibwa Sugar huku akimalumu kiungo Abdulaziz Makame akimtaka kubadilika.

Likungwa amesema Makame anatakiwa kubadilika haraka na kuacha kucheza kwa masikhara ambapo hakuonyesha umakini na utulivu katika kupiga penalti.

Naye Robert Joseph amesema hajaelewa kwanini makocha wa timu hiyo hawakupanga kikosi kamili huku kukiwa na wachezaji nyota katika benchi ambao hawakupewa nafasi.

Amesema hatua hiyo pekee inaonyesha ni jinsi gani timu yake ilidharau mechi hizo na kuwaumiza mashabiki wengi.

Hata hivyo kocha msaidizi wa Yanga, Said Maulid ametolea ufafanuzi hoja hizo akisema vijana wake hawakudharau mechi hiyo na kwamba walipambana lakini hawa kufanikiwa kushinda.

Chanzo: mwananchi.co.tz