Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbegu amhatarishia namba beki Singida BS

Yahaya Mbegu To Simba yahya Mbegu atajwa kutua Singida Big Stars

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa kushoto Yahya Mbegu anatajwa kutua Singida Big Stars basi Yassin Mustapha huenda akapoteza namba endapo dili hilo likakamilika.

Mbegu amekuwa na msimu bora hadi kuitwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na inadaiwa Simba nao wamempa mkataba beki huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Tayari SBS ina Shafiq Batambuzi ambaye Kocha Hans Van Pluijm amekuwa akimwanzisha kikosi cha kwanza huku Mustapha ambaye amewahi kuichezea Yanga, Polisi Tanzania na Ndanda akisubiri.

Mwanaspoti limedokezwa kuwa mkataba huo wa Mbegu na Singida ni wa miaka miwili na kwamba benchi la ufundi lilikuwa linamhitaji mno beki huyo.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo ni kwamba beki huyo na nyota wengine wanasajiliwa kwa sasa kwa ajili ya michuano ya CAF ya msimu ujao baada ya timu hiyo kujihakikisha kutaka tiketi ambapo itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ndani ya Ihefu, Mbegu amekuwa chaguo la kwanza la timu hiyo na mchango wake umeifanya timu hiyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuepuka kushuka daraja tofauti na ilivyokuwa mwishoni mwa duru la kwanza la msimu huu ilipokuwa ikiburuza mkia.

Uwepo kwa Mustafa na Batambuze ulichangia kumfanya beki chipukizi Nickson Kibabage kuhamishwa eneo la mbele akicheza kama winga ambaye kwa sasa anatajwa yupo mbioni kutua Yanga.

Kiungo wa zamani wa Kagera Sugar na Milambo ya Tabora, Shaka Titus alisema Mustapha anatakiwa kupambana ili kupata namba kwani Mbegu ni mchezaji mzuri na amekamilika kila idara.

“Kwa mchezaji hapo ndio unatakiwa kuonesha sasa uwezo wako, sina wasiwasi na Mustapha lakini anatakiwa kupambana,” alisema Titus

Chanzo: Mwanaspoti