Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe na mshahara wake Madrid kafunikwa

Mbappe X Mshaharaaa Mbappe na mshahara wake Madrid kafunikwa

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ndo hivyo. Kuna mastaa kibao kwenye Ligi Kuu England wanalipwa mshahara mkubwa kuzidi anaolipwa Kylian Mbappe huko Real Madrid.

Mabingwa hao mara 15 wa Ulaya, Real Madrid walithibitisha kunasa saini ya Mbappe kwa kumsainisha dili la miaka mitano. Fowadi huyo wa kimataifa wa Ufaransa ataungana rasmi na wenzake Julai 1, siku moja baada ya mkataba wake kufika ukomo Paris Saint-Germain.

Mbappe, 25, alieleza mapema mwaka huu kwamba itakapofika majira ya kiangazi ataachana na PSG. Akiwa mchezaji huru na kufahamika kama mmoja wa mastraika bora kabisa duniani, Mbappe ameripotiwa kulipwa ada ya usajili, ambayo ni kati ya Pauni 80 milioni hadi Pauni 128 milioni.

Hata hivyo, mshahara wake wa wiki, unaripotiwa kuwa ni kama Pauni 250,000 baada ya kodi -- kwa mchezaji wa kariba yake, kiwango hicho ni kidogo kwa sababu kuna mastaa wasiopungua 10 kwenye Ligi Kuu England wanalipwa mshahara mkubwa kumzidi.

Anayeongoza kwenye orodha hiyo ya mastaa wenye mishahara mikubwa kwenye Ligi Kuu England ni kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne, anayelipwa Pauni 400,000 kwa wiki, wakati mchezaji mwenzake huko Etihad, Erling Haaland, anafuatia, akiwa analipwa Pauni 375,000 kwa wiki kwa mujibu wa Spotrac.

Wachezaji wa kwanza ambao si wa Man City kwenye orodha ya wanaolipwa mshahara mkubwa ni kiungo wa Manchester United, Casemiro na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, ambao kila mmoja analipwa Pauni 350,000 kwa wiki.

Kuna mastaa wawili wa Chelsa wanafuatia kwenye orodha hiyo, licha ya kwamba ni mmoja tu ambaye amekuwa akiichezea klabu hiyo ya Stamford Bridge, licha ya kuwa kwenye sintofahamu kubwa, huku mwingine akiwa anazurura tu kwa kutolewa kwa mikopo. Wakali hao ni Raheem Sterling na Romelu Lukaku, ambao kila mmoja analipwa Pauni 325,000 kwa wiki.

Kisha wanafuatia mastaa wengine wawili wa kutoka Man City, Bernardo Silva na Jack Grealish, pamoja na fowadi wa Man United, Marcus Rashford, ambao kila mmoja analipwa Pauni 300,000 kwa wiki. Anayekamilisha 10 bora ni staa wa Arsenal, ambaye ndiye pekee wa kutoka kwenye kikosi hicho cha Emirates, aliyeingia kwenye orodha hii ya wanaolipwa mshahara mkubwa kumzidi Mbappe, ambaye ni Kai Havertz, anayelipwa Pauni 280,000 kwa wiki.

Kutokana na bonasi yake atakayolipwa kwenye ada ya usajili, Mbappe hawezi kutishika sana na malipo ya mshahara wa kila wiki. kuthibitishwa kwake kwamba ni mchezaji mpya wa Real Madrid kumefichua siri kubwa inayoweza kufanyika kwenye soka baada ya staa huyo wa zamani wa AS Monaco kuhusishwa sana na mpango wa kwenda Bernabeu, lakini muda wote alipiga kimya.

Mbappe kwa sasa yupo kwenye kambi ya kikosi cha Ufaransa kinachojiandaa na mikikimikiki ya Euro 2024 na baada ya fainali hizo kufika tamati atakwenda kujiunga na timu yake mpya ya Real Madrid.

Aliandika kwenye mtandao wa X: “Ndoto imekuwa kweli. Ni furaha kubwa na najivunia kuwa sehemu ya klabu ya ndoto zangu, Real Madrid. Ni ngumu kuelezea furaha na hisia ninazojisikia kwa sasa.”€

Chanzo: Mwanaspoti