Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe majanga, Kocha asema anaweza asione tena

Mbappe France Mask Kylian Mbappe

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amefunguka na kubainisha wasiwasi wake juu ya mchezaji Kylian Mbappe kucheza akiwa amevaa maski, hilo linaloweza kumfanya asiwe na uono mzuri kwenye fainali za Euro 2024.

Mbappe alivunjika pua kwenye mechi ya kwanza ya Ufaransa ilipokipiga na Austria, lakini siku za karibuni alionekana kufanya mazoezi akiwa amevaa maski na ilitazamiwa kama usiku wa jana Jumanne, angecheza kwenye mchezo dhidi ya Poland.

Alikosa mechi ya Uholanzi, hivyo mashabiki walimsubiri kwa mchezo wa jana dhidi ya Poland uliopaswa kufanyika huko Dortmund.

Alipoulizwa kama maski itakuwa na msaada kwa supastaa huyo, Deschamps alisema: “Kupumua sio shida, lakini kuona nadhani itakuwa shida. Sijawahi kucheza na maski, lakini navuta hisia kwa wale wanaovaa, nahisi kama hawapo na uhuru sana.

“Nachokiona ni kama kinazuia kidogo uono wako. Ni wazi kunakuwa na vikwazo kwenye uono.”

Kocha Deschamps aliulizwa alishindwa kuweka mambo hadharani kuhusu mshambuliaji huyo kama angetumika kwenye mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Poland, ambayo tayari imeshaaga fainali hizo za Euro 2024.

“Anaendelea vizuri siku hadi siku,” alisema Deschamps.

“Juzi tulikuwa wote mazoezini na majeraha yake kwenye pua yalionekana kukauka. Itamlazimu kuzoea kucheza na maski. Yeye anataka kucheza kila mechi, alitaka kucheza ile ya Uholanzi na alitaka pia kucheza dhidi ya Poland.”

Kabla ya mchezo wa usiku wa jana, Ufaransa ilikuwa imefunga bao moja tu kwenye Euro 2024, tena bao lenyewe ni la mchezaji wa Austria, Maximilian Wober kujifunga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live