Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe kutangazwa muda wowote Real Madrid

Skysports Kylian Mbappe Psg 6462523 Kylian Mbappe

Sun, 2 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Real Madrid imeripotiwa itamtambulisha Kylian Mbappe kuwa usajili wa kwanza dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, kesho, Jumatatu.

Kikosi hicho cha kocha Carlo Ancelotti, usiku wa jana Jumamosi kilikuwa na kibarua cha kukabiliana na Borussia Dortmund kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Wembley.

Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la L’Equipe, Real Madrid ilipanga kumtambulisha Mbappe kuwa usajili wa kwanza kwenye dirisha hili saa chache mbele baada ya fainali ya Ulaya.

Taarifa zilidai Mbappe atatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Real Madrid, Jumatatu, huku ikitambua hilo haliwezi kuwa na athari hasi Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2024, ambapo mchezo wa kwanza watakipiga Juni 17. Mbappe, amefunga mabao 256 na asisti 108 katika mechi 308 alizochezea PSG.

ARSENAL imepata pigo kwenye mchakato wa kunasa huduma ya straika wa Inter Milan, Lautaro Martinez baada ya mkali huyo kusisitiza hataki kung’oka Italia. Arsenal iliriporiwa kuvutiwa na huduma ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina, lakini yupo kwenye hatua za mwisho za kusaini dili jipya la kuendelea kukipiga Inter Milan. Arsenal ipo sokoni kusaka straika dirisha hili.

CHELSEA ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la kunasa saini ya beki wa Fulham, Tosin Adarabioyo kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kwa muda sasa kumekuwa na ripoti juu ya Chelsea kuhitaji saini ya beki huyo, ambaye atakuwa huru kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake huko Fulham kufika tamati.

KOCHA Antonio Conte ameripotiwa kuwa na mpango wa kuvamia Chelsea kwenda kunasa huduma ya straika Romelu Lukaku dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kocha huyo atachukua mikoba kuinoa Napoli kwa miaka mitatu. Ripoti zinafichua Conte anahitaji saini ya Lukaku akiamini atakwenda kuziba pengo la Victor Osimhen, endapo kama atahama.

MANCHESTER United imehamishia nguvu kunasa saini ya beki wa pembeni wa Bournemouth, Milos Kerkez. Man United inataka kujiimarisha kwenye beki ya kushoto baada ya Luke Shaw na Tyrell Malacia kusumbuliwa na majeraha msimu wote uliopita. Ripoti zinafichua kwamba Man United inahitaji saini ya Kerkez dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

JUVENTUS imeripotiwa kupewa ofa ya kumsajili kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz dirisha hili. Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, staa huyo anayedaiwa kuwa na thamani ya Pauni 40 milioni, amewekwa kwenye mipango ya miamba hiyo ya Italia. Juventus imepanga kumjumuisha kwenye dili la kuwavutia zaidi Aston Villa ili wamruhudu Luiz akakipige Turin.

ARSENAL imeripotiwa kugonga mwamba kwenye mchakato wa kunasa huduma ya kiungo mkabaji, Martin Zubimendi kwenye dirisha hili la kiangazi. Kocha Mikel Arteta alimuweka kiungo huyo kwenye orodha ya wachezaji anaotaka kuwanasa, lakini shida inayoibuka ni kwamba mkali huyo wa Real Sociedad mipango yake ni kwenda Barcelona.

TOTTENHAM Hotspur imeripotiwa kuwa na mpango wa kuwafungulia mlango wa kutokea mastaa wake 11 akiwamo kiungo mkali, Pierre-Emile Hojbjerg. Mchakato huo umepangwa kufanyika dirisha hili la kiangazi ambapo kwenye orodha hiyo ya mastaa watakaopigwa bei itawahusu pia Richarlison, Emerson Royal, Bryan Gil na Giovani Lo Celso.

Chanzo: Mwanaspoti