Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe kutambulishwa Santiago Bernabéu Julai 16, ataa jezi ya Ronaldo na Modrick

Bernabeuuu E4.jpeg Mbappe kutambulishwa Santiago Bernabéu Julai 16, ataa jezi ya Ronaldo na Modrick

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid imetangaza kuwa itamtambulisha nyota wao mpya Kylian Mbappé katika dimba la Santiago Bernabéu mnamo Julai 16, 2024.

Mbappé alijiunga na Madrid kwa mkataba wa miaka mitano msimu huu wa joto baada ya mkataba wake kumalizika Paris Saint-Germain, na hivyo kumaliza harakati za miamba hao wa LaLiga kumnasa mchezaji huyo.

Mashabiki wa Madrid wanatarajiwa kuujaza uwanja wa Bernabéu wenye uwezo wa kujaza mashabiki 81,000 kwa ajili ya utambulisho wa Mbappé, katika tukio ambalo linatajwa kuwa litakuwa kubwa kwa klabu hiyo tangu kutambulishwa kwa Cristiano Ronaldo mwaka 2009.

Ufaransa ya Mbappé ilitolewa na Uhispania katika nusu fainali ya Euro 2024 wiki hii, baada ya mshambuliaji huyo kuvunjika pua katika mchezo wake wa kwanza wa michuano hiyo na kufunga bao moja pekee dhidi ya Poland katika mechi tano.

Baada ya kuvunjika pua dhidi ya Austria, Mbappé alivaa kinyago cha kujikinga katika michezo ya Ufaransa ya Euro 2024 dhidi ya Poland, Ubelgiji na Ureno, kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 Jumanne dhidi ya Uhispania.

Madrid ilitangaza kumsajili Mbappé mnamo Juni 3, na hivyo kuhitimisha moja ya sakata za uhamisho wa muda mrefu zaidi katika soka.

Mbappé alikaribia kujiunga na Madrid kabla ya kuhamia PSG kutoka Monaco mwaka 2017, na tena mwaka wa 2022, wakati mabadiliko ya dakika za mwisho yalipomwona akisaini mkataba mpya huko Paris.

Madrid wamethibitisha kuwa mshambuliaji wao Kylian Mbappe atavaa jezi namba 9. Cristiano Ronaldo alivaa jezi hiyo pia, alipowasili klabuni hapo mwaka 2009 kabla ya kubadili na kuvaa namba 7. Mbappe inasemekana aliamua kutoomba namba 10, ambayo anavaa kwenye timu ya Taifa ya Ufaransa, kwa heshima ya Luka Modric.

Hata hivyo, Mbappe atalazimika kuwapa vionjo mashabiki wa Madrid akiwa na jezi namba 9, ambayo imewahi kuvaliwa na Mreno na Mbrazil Ronaldo, Karim Benzema, Emilio Butragueno na Alfredo Di Stefano.

Mbappe aliondoka PSG na rekodi ya kushangaza ya mabao 256 na asisti 108 katika michezo 308 na kumfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa PSG akishinda mataji 6 ya Ligue 1 na kutajwa kuwa mchezaji bora wa Ligue 1 mara tano. Amefunga mabao 48 katika mechi 84 alizoichezea Ufaransa.

Madrid wanaelekea Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo watacheza na AC Milan, Barcelona na Chelsea, kabla ya fainali ya UEFA Super Cup dhidi ya Atalanta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live