Mshambulizi wa Ufaransa Kylian Mbappe ameiambia Paris St-Germain kuwa ana nia ya kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na mabingwa hao wa Ligue 1 umepangwa kumalizika na amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Real Madrid.
Mustakabali wa Mbappe ulikumbwa na mzozo mkubwa na PSG msimu uliopita wa joto.
Wakati fulani, Mbappe alifukuzwa kwenye kikosi cha kwanza na kuachwa nje ya ziara ya klabu hiyo ya maandalizi ya msimu mpya barani Asia.
Walakini, makubaliano yalifikiwa ambayo yalihakikisha PSG haitapoteza wakati Mbappe hatimaye ataondoka na masharti ya kuondoka kwake ambayo sasa inaonekana hauwezo kuepukika bado yanathibitishwa.
Mshambulizi huyo ana kipengele cha kuongeza mwaka mmoja, hivyo inatarajiwa kuondoka kwake kutahusisha ama mauzo na ada ya uhamisho au fidia za kifedha kwa upande wa mchezaji.
Ingawa PSG wangetaka Mbappe abaki klabuni hapo, kuondoka kwake kunaonekana kuja huku wakilenga kujenga kikosi cha vijana na kuachana na mpango wa 'Galacticos', ambao pia umewafanya fowadi wa Argentina Lionel Messina Mbrazil Neymarkuondoka tangu wakati hu.
Inakadiriwa Mbappe, ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa mwaka 2018, anapokea takriban €200m kwa mwaka (£171m).