Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe aweka rekodi zake PSG, wakati Mkataba ukielekea ukingoni

Mbappe PSG 768x432 Kylian Mbappe

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya PSG, Kylian Mbappe amefanikiwa kuandika rekodi mpya na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufikisha magoli 100 ya Ligue 1 akiwa na klabu hiyo.

Mbappe, 22 amerandika rekodi hiyo baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya timu yake ya zamani ya Monaco katika mchezo wa Ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Mchezaji huyo anaandika Rekodi hiyo tangu Opta ilivyoanza kuandika rekodi hizo mwaka 1950/51 akiweka rekodi hiyo akiwa na miaka 22 na siku 357.

“Napenda kucheza. Napenda kucheza, Bado napenda kuwepo uwanjani kucheza kila mchezo,” Mbappe alisema baada ya ushindi. “Hivyo ni heshima kuweza kucheza tena leo, kuweza kusaidia timu yangu. natumai nitaendelea hivi katika mechi zote za msimu huu.

“Ni mpira! Siku zote nasema nilikuwa na muda mzuri nilipokua [Monaco]. Nilikulia hapo. Na kumbukumbu nzuri. Lakini kurasa zimegeuka. Nacheza PSG, Ninafuraha. Nafanya kila kitu kwaajili ya klabu.” aliongeza.

Ikumbukwe mkataba wa Mbappe na PSG unakamilika mwishoni mwa msimu huu wakati mpaka sasa hajasaini mkataba mpya, huku tetesi zikimuhusisha na kujiunga na Real Madrid ya Uhispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live