Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe ataka 14 waondoke PSG, wamo Neymar, Pochettino

Mbappe N Neymar Mbappe na Messi

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameripotiwa kuwa na orodha ya watu 14 ambao anataka waondoke ndani ya timu hiyo akiwemo Kocha wake Mauricio Pochettino na Neymar.

Kinda hilo lenye umri wa miaka 23 pekee, Mbappe mapema wiki iliyopita alisaini mkataba mpya na PSG ambao umempa mamlaka makubwa mno ili kuachana na mpango wake wa kujiunga na Real Madrid huku kandarasi hiyo ikimuhakikishia kitita kizito cha paundi 650,000 kwa wiki ndani ya matajiri hao wa Ufaransa.

Mbappe amepewa mamlaka makubwa hata katika sajili zitakazofanyika PSG na hivyo inadaiwa Mfaransa huyo anaanza na dirisha hili.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, ajira za watu 14 zipo mashakani kutokana na mshindi huyo wa Kombe la Dunia anahitaji kukisafisha kikosi cha PSG.

Panga la Mbappe linawahusu viungo Julian Draxler, Ander Herrera, Idrissa Gueye, Mauro Icardi, Leandro Paredes​ ana Thilo Kehrer.

Wengine ambao wapo kwenye orodha ya Kylian Mbappe ni pamoja na Danilo Pereira, Layvin Kurzawa, Pablo Sarabia​, Juan Bernat, Colin Dagba​ na Sergio Rico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live