Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe apiga bao Hat-trick, Kocha hajafurahia

Mbappe With Enrique Mbappe apiga bao Hat-trick, Kocha hajafurahia

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Kylian Mbappe siku ya jana kufunga mabao 3 (hat-trick) kwenye mchezo wa Ligue 1, (REIMS 0-3 PSG) bado kocha wake Luis Enrique ameonyesha kutofurahishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo, katika mahojiano na vyombo vya habari Enrique alinukuliwa akisema.

“Sifurahishwi na Kylian Mbappe, sina la kusema kuhusu mabao, lakini anaweza kuisaidia timu kwa namna nyingine, nitazungumza naye kwanza lakini ni mazungumzo ya faragha, Kylian ni mmoja. ya wachezaji bora zaidi duniani, lakini tunataka zaidi. Tunataka afanye zaidi,"

Lakini pia kuna tetesi kuwa baadhi ya wachezaji wa klabu ya PSG wanamuona Mbappe ni mchezaji ambaye hapambani kwa ajili ya klabu na badala yake anajipambania mwenyewe kwa maslai binafsi, minong'ono iliaza mara baada ya PSG kupokea kichapo cha bao 2-1 dhidi ya AC Milan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live