Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe apewa jezi namba 9 kwa masharti Real Madrid

Mbappe X Benzema Jezi Kylian Mbappe

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ya kutambulishwa kama mchezaji mpya ndani ya Real Madrid imefahamika kuwa Kylian Mbappé atavaa jezi namba 9 kwa kuwa jezi yake pendwa ya namba 10 ipo mgongoni mwa kiungo fundi mkongwe Luka Modric.

Kutokana na heshima ambayo Modric anayo ndani ya miamba hiyo ya Uhispania ataendelea kuvaa jezi namba 10 mpaka atakapoondoka au kutundika daluga mwisho wa msimu ujao ndipo jezi hiyo itakuwa huru.

Hivyo Mbappé ataendelea kusubiri jezi hiyo kama ilivyokuwa kwa Ronaldo miaka kadhaa nyuma wakati jezi namba 7 ilipokuwa inavaliwa na mkongwe wa wakati huo, Raul Gonzalez.

Itakumbukwa Cristiano Ronaldo alivaa jezi namba 9 kwa msimu mzima wa 2009/10 alipojiunga na Real Madrid mnamo 2009 kwasababu jezi yake pendwa ilikuwa inavaliwa na gwiji Raul Gonzalez na alikabidhiwa jezi namba 7 mwanzoni mwa msimu wa 2010/11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live