Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe aomba kuondoka PSG

B0231595 901E 4C4D 84CA 19F28E7058AF.jpeg Kylian Mbappe

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ameomba kuondoka klabuni hapo katika dirisha dogo la januari.

Tetesi zinasema Kylian Mbappe anahitaji kuondoka klabuni hapo kutokana na kutokuelewana na uongozi wa klabu hiyo kwenye baadhi ya makubaliano ndani ya timu hiyo.

Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema inawezekana klabu ya Real Madrid ikarudi kwenye mbio za kumnasa mchezaji huyo waliemkosa majira ya joto baada ya kusaini mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo mpaka 2024.

Kylian Mbappe amekua akielezwa kupishana na wachezaji wenzake klabuni hapo na hiyo ni baada ya taarifa kuvuja kua mchezaji huyo alisaini mkataba unaompa mamlaka makubwa klabuni hapo uwanjani na nje ya kiwanja.

Klabu zingine pia zimehusishwa kumuwania mchezaji huyo baada ya taarifa hiyo kutoka ikiwemo klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live